BEI YA MAFUTA YA ALIZETI NA MASHUDU YAKWEA MLIMA KILIMANJARO !

BEI YA MAFUTA YA ALIZETI NA MASHUDU YAKWEA MLIMA KILIMANJARO !

Bei ya mafuta ya alizeti na mashudu kwa mwezi Novemba yazidi kupanda juu hata katika mikoa ambayo alizeti inalimwa kwa wingi.Kuelekea mwisho wa mwaka mazao mengi hupanda bei.

Kwa sasa mkoani Dodoma bei ya jumla ya lita moja ya mafuta ya alizeti ni TZS 6000; wakati mashudu yanauzwa kwa bei jumla ya TZS 800 kwa kilo moja.

Bei hizi zinategemewa kuendelea kupanda zaidi hadi mwezi May/June mwakani ambapo mavuno yataanza na kwa wastani mafuta ya alizeti wakati wa mavuno huuzwa kati ya  TZS 3,000 hadi 4,000 kwa lita (bei ya jumla). Na mashudu ya alizeti huuzwa kati ya TZS 250 -400 kwa kilo 1 (kwa jumla) wilayani hapa.

Kwa upande wa IRINGA mjini mafuta ya alizeti ni TZS 6000/lita (bei ya jumla) na mashudu ni TZS 600 -700/Kg mkoani humo.

Je ungehitaji kununua au kuuza mazao ya kilimo na mifugo? Aina gani? Tuandikie hapa.

Back to blog

Leave a comment