HUDUMA YA KUTEMBELEWA SHAMBANI & USHAURI/EXTENSION SERVICES

Kutembelea shamba(farm survey) ni kazi ya mwanzo kabisa ambayo inatakiwa kufanyika hata kabla ya kununua shamba lenyewe au kama hukufanya hivyo basi inatakiwa kufanywa kabla ya kuanza kuwekeza katika shamba hilo.

Faida za kutembelea shamba kitalaam:-

1.Kujua historia ya shamba lenyewe

2.Kutathimini uoto wa asili na tabia za udongo kwa mwonekano na muundo

3.Kutambua miundombinu na fursa zilizopo shambani

4.Kung'amua changamoto zilizopo za kimazingira na kijiografia mapema na kutengeneza mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo shambani.

5.Kuandaa ripoti ya tathmini ya shamba,miundombinu,changamoto na ushauri kabla ya hata kuanza kuandaa bajeti ya uendeshaji wa mradi husika.

Kabla ya kutembelewa shambani sharti ujaze fomu ya kuomba kutembelewa shambani; ni vizuri zaidi kutuma maombi haya angalau siku 3 kabla ya kutembelewa shambani ili uweze kupangiwa siku ya kutembelewa shambani.

Unaweza kutumia usafiri wako kuwapeleka wataalam wetu shambani au kuwalipia usafiri wa umma utakaowawezesha kwenda na kurejea kutoka shambani;na ikiwa itawalazimu kulala huko shambani ni muhimu kuweka mipango mapema ya kuwapatia malazi na chakula kwa muda wa kazi hiyo.

Baada ya kazi ya survey utapatiwa ripoti kamili ya ukaguzi wa shamba ikionesha fursa,changamoto na ushauri juu ya aina gani ya mazao yanayopendekezwa na mbinu stahiki za kufuata ili kufanya mradi/miradi yako .Mapendekezo haya yanaweza kuhitaji kupima afya ya udongo,kuchimba kisima au kubadili aina ya mradi.Gharama za kupima afya ya udongo na nyinginezo za shambani baada ya survey zitakuwa juu ya mmiliki wa shamba na hazitakuwa sehemu ya ada ya kutembelewa shambani.

Ripoti ya ukaguzi wa shamba itatumwa kwa mmiliki wa shamba au meneja wa mradi husika ndani ya siku 2-3 za kazi tangu kutembelewa shambani.

Wakati wa kutembelea na kukagua shamba utaruhusu zichukuliwe picha nyongevu(videos) kwa ajili ya rejea wakati wa kuandika ripoti.

Gharama za kutembelea shamba hutegemea ukubwa wa shamba,umbali lilipo shamba,hali ya sasa ya shamba (msitu/limelimwa) n.k.Gharama hizi hulipwa baada ya kujaza fomu na kujibiwa ni kiasi gani utalipa na lini kazi hii itafanyika.Malipo haya hufanyika siku moja kabla ya kwenda katika shamba husika.

Huduma za Ugani

Huduma za ugani ni kipande muhimu katika maendeleo ya kilimo na ustawi wa jamii. Zinachangia katika kuboresha uzalishaji wa mazao, kuongeza tija na kusaidia wakulima kupata maarifa na ujuzi mpya. Kwa kupitia huduma hizi, wakulima wanapata msaada wa kitaalamu katika masuala mbalimbali kama vile mbinu bora za kilimo, usimamizi wa rasilimali, na mbolea bora.

Huduma za ugani pia husaidia katika kukuza uelewa wa wakulima kuhusu masuala ya soko, mabadiliko ya tabianchi, na teknolojia mpya zinazoweza kuboresha uzalishaji. Hii ni muhimu sana katika kuhakikisha wakulima wanakuwa na uwezo wa kujikimu na kuendeleza shughuli zao kwa njia endelevu.

Utaratibu wa Huduma za Ugani na Ushauri

Ili kuhakikisha huduma za ugani zinafanya kazi kwa ufanisi, utaratibu ufuatao utatumika:

  1. Ufuatiliaji wa Mahitaji: Kwanza, wataalamu wa ugani watafanya tathmini ya mahitaji ya wakulima katika eneo husika. Hii itajumuisha mikutano ya hadhara, mahojiano na wakulima, na uchambuzi wa taarifa za kilimo.

  2. Kujenga Uhusiano: Wataalamu wa ugani watajenga uhusiano mzuri na wakulima ili kuweza kuelewa changamoto wanazokabiliana nazo na kuwa na njia bora za kutoa msaada.

  3. Kutoa Mafunzo: Mafunzo yataandaliwa kwa wakulima kuhusu mbinu za kisasa za kilimo, usimamizi wa mazao, na matumizi sahihi ya rasilimali. Mafunzo haya yanaweza kufanyika kupitia warsha, semina, au hata kwa njia ya mtandao.

  4. Usimamizi wa Maendeleo: Wataalamu wa ugani watakuwa na jukumu la kufuatilia maendeleo ya wakulima na kutoa ushauri wa mara kwa mara ili kuhakikisha kwamba mikakati inatekelezwa ipasavyo.

  5. Kutoa Rasilimali na Vifaa: Katika baadhi ya matukio, huduma za ugani zinaweza kusaidia katika upatikanaji wa mbolea, mbegu bora, na vifaa vya kilimo ili kuboresha uzalishaji wa wakulima.

  6. Kuhamasisha Ushirikiano: Huduma za ugani zitahamasisha wakulima kushirikiana katika vikundi ili kuongeza nguvu na uwezo wao wa kujadiliana na masoko.

Kwa kufuata utaratibu huu, huduma za ugani zitaweza kutoa msaada wa maana kwa wakulima na kuchangia katika maendeleo endelevu ya sekta ya kilimo katika jamii.

Ni muhimu kutembelea shamba kabla ya kuwekeza ili kuweza kupanga vizuri uendeshaji wa mradi wako.

Jaza fomu ya maombi ya kutembelewa leo na wataalam wetu walio maeneo yote nchini na upate kulima kitaalamu.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa: WhatsApp +255 757 757 968 ; Email: info@aje-farms.com