ZIARA ZA MASHAMBANI/VIWANDANI/MAONESHO MBALIMBALI
Ili kuhakikisha tunatoa huduma zetu kwa vitendo kwa walengwa tutaratibu na kufanya ziara mbalimbali ndani na nje ya Tanzania katika viwanda,mashamba na maonesho mbalimbali ; kwa lengo la kukuza uelewa na kutengeneza mtandao wa kibiashara katika mnyororo wa thamani wa kilimo na ufugaji.Tutashirikiana na sekta za umma na binafsi ili kutimiza azma hii muhimu ili kuleta mapinduzi makubwa kwenye KILIMO BIASHARA.
Wakati wa ziara washiriki watajifunza,kuelimishwa juu ya teknolojia,zana na mbinu mbalimbali za kitaifa,kikanda na kimataifa juu ya kilimo biashara.
Kupitia ziara hizi washiriki watatengeneza mahusiano ya kibiashara baina yao na wafanyabiashara/wakulima na wadau mbalimbali katika maeneo waliotembelea.
Kila mshiriki atalipa ada ya ziara husika kwa kutegemea eneo/nchi/mkoa/wilaya ziara itakapofanyika.Ada hii itapangwa na mratibu wa ziara kwa kuzingatia vigezo vyote muhimu na inaweza kuhusisha nauli,chakula,malazi na uratibu wa ziara.
Kabla ya kushiriki ziara husika ni muhimu kuomba kushiriki katika ziara hiyo kwa kujaza fomu ya ushiriki mapema iwezekanavyo ili kufanya kazi ya mipango ya ziara husika kuwa nyepesi.
Unaweza kujifunza maarifa kwa siku 1 kupitia kutembea kuliko kukaa darasani kupata maarifa hayo kwa miaka 10 ! Tembea uone na ujifunze.
Je ungependa kutembelea shamba/kiwanda gani? -Mkoa/Wilaya/Nchi gani?
JAZA FOMU LEO !
Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana nasi kwa : WhatsApp+255 757 757 968 : Email: info@aje-farms.com