WAANDISHI WA KUJITEGEMEA

Katika dunia inayoenda kwa kasi kidijitali uwepo wa intaneti na ukuaji wa TEHAMA unampa kazi kila mmoja kama atakuwa na fikra sahihi. TEHAMA imeongeza kazi kwa mamilioni ya ambao hawakuwa na kazi.

Kwa sasa ni rahisi kufanya kazi ukiwa na simu na intaneti tu. 

AJE-FARMS;MASHAMBA YANAYOTEMBEA tunaamini katika TEHAMA ili kukuza masoko na elimu ya kilimo biashara.

Ili kutimiza azma hii basi tunatoa fursa sawa kwa yeyote mwenye uwezo wa kutumia simu yake janja (smartphone) kamera kukusanya,kuchakata(editing) na kutuma taarifa mbalimbali za kilimo na ufugaji kutoka popote duniani.Taarifa hizi zikishatumwa kwetu zitahaririwa na kisha kuchapishwa katika majukwaa mbalimbali ya mitandao ya kijamii kwa lengo la kusambaza TAARIFA kwa jamii yenye uhitaji mkubwa wa taarifa hizi. Dunia ya sasa hivi inaendeshwa na taarifa na hata SOKO ni TAARIFA ! Uwepo wa taarifa sahihi kwa wakati utawezesha wakulima,wafugaji,wafanyabiashara kuweza kutekeleza shughuli zao kwa ufanisi wa hali ya juu na hivyo kukuza uchumi wa taifa.Ni dhahiri TAARIFA NI SILAHA.

Tunakaribisha maombi ya waandishi wa kujitegemea ambao watalipwa kwa kuzingatia kiasi cha taarifa na aina ya taarifa wanazokusanya na kisha kuzituma AJE-FARMS;MASHAMBA YANAYOTEMBEA.Waombaji wote watatakiwa kuwa na uwezo,utashi,weledi,maadili stahiki ili kuweza kukubaliwa kufanya kazi hii.

Ili kuomba nafasi ya kuwa mwandishi wetu wa kujitegemea tafadhali jaza fomu ya maombi ya kazi na ukikubaliwa utafanyiwa usahili kabla ya kuanza kazi hii.

Unasubiri nini ? Jaza fomu ya maombi leo ! 

Kwa maelezo zaidi WhatsApp :0757 757 968 au Email: info@aje-farms.com