MASHAMBA DARASA/WAUZAJI WA MAZAO YA KILIMO NA MIFUGO WALIOSAJILIWA
Shamba Darasa ni mradi unaotarajia kuweka takwimu halisi za wakulima na wafugaji maeneo mbalimbali zikionesha ukubwa wa mashamba yao,miradi iliyopo ,uwezo wao wa kuzalisha,kalenda zao za kuzalisha,fursa na changamoto zilizopo katika mashamba yao.
Kwa kufanya hivyo itakuwa rahisi kushawishi masoko ya ndani na nje ili yanunue mazao yao.
FAIDA KWA MMILIKI WA SHAMBA DARASA:
1)Shamba husika litatangazwa na AJE-FARMS pamoja na washirika wake
2)Wafanyakazi wa shamba husika watapatiwa mafunzo juu ya kilimo na ufugaji kwa kufuata kanuni sahihi za uzalishaji ili kulinda ubora wa mazao yanayokidhi vigezo vya masoko ya ndani na nje.
3)Mmiliki atapata asilimia 50% ya ada za mafunzo shambani wakati asilimia 50% ya ada hiyo ikilipwa kwa AJE-FARMS
4)Kupitia matangazo shamba litapata wateja wa mazao yanayozalishwa hapo shambani na pia hii itavutia wawekezaji shambani
IKUMBUKWE:
Ili kuleta ufanisi mashamba darasa yote yatakuwa chini ya uratibu na ushauri wa AJE-FARMS pamoja na washirika wake na hivyo ili kuweza kufika katika shamba darasa husika inafaa kuwasiliana na AJE-FARMS kwa WhatsApp 0757 757 968 ikiwa unahitaji kwenda kujifunza,kununua mazao au kuwekeza katika shamba darasa husika.
Mali zote za shambani zitabakia chini ya umiliki wa mwenye shamba husika na wafanyakazi wote wa shamba hilo wataajiriwa na kulipwa na mmiliki wa shamba.
SAJILI SHAMBA LAKO LEO NA UPATE FAIDA LUKUKI ! JAZA FOMU YA KUSAJILI SHAMBA LAKO KWA DAKIKA 2 TU hapa :
FOMU YA KUSAJILI SHAMBA DARASA
https://myh1nx-4b.myshopify.com/pages/fomu-ya-kusajili-shamba-darasa
YAFUATAYO NI MASHAMBA DARASA YALIYOSAJILIWA NA AJE-FARMS:-
1.SHAMBA DARASA LA UFUGAJI NYUKI WANAOUMA NA WASIOUMA LILILOPO DONGE -ZANZIBAR
2.SHAMBA DARASA LA UFUGAJI WA KUKU KIENYEJI MBEGU NDEFU YENYE UZITO MKUBWA LILILOPO MAGU-MWANZA
3.SHAMBA DARASA LA KILIMO MSETO NA UFUGAJI LILILOPO KISARAWE-PWANI
4.SHAMBA DARASA LA UFUGAJI MSETO LILILOPO RUNGWE-MBEYA
5.SHAMBA DARASA LA KILIMO CHA MPUNGA MAGU-MWANZA
6.SHAMBA DARASA LA KILIMO CHA NYANYA NA ALIZETI LILILOPO MVOMERO-MOROGORO
7.SHAMBA DARASA LA KILIMO CHA CHIKICHI,EMBE,FENESI NA MITI YA MBAO PAMOJA NA UFUGAJI WA SAMAKI NA NYUKI LILILOPO BAGAMOYO -PWANI
8.SHAMBA DARASA LA KILIMO CHA PASHENI,PARACHICHI,PAPAI NA PILIPILI KICHAA LILILOPO NAMPALAHALA -BUKOMBE MKOANI GEITA