BEI YA MCHELE YAZIDI KUPANDA
Share
Katika soko la Kahama kama yalivyo maeneo mengine nchini bei ya mchele inazidi kupanda na hali hii ilitegemewa .
Kwa sasa bei ya kilo 1 ya mchele mjini Kahama ni kati ya TZS 1,600 - 2500 kulingana na ubora na daraja mchele.Bei hii haitofautiani na maeneo mengine mengi kanda ya Ziwa;ambayo hufanya kilimo cha mpunga kwa kiasi kikubwa.
Hata hivyo bei ya mchele hushuka kila mwaka kati ya mwezi wa 4 hadi wa 6 ambapo ndio kipindi cha mavuno maeneo mengi nchini ;na bei ya mchele mjini hapa huwa kati ya TZS 800 -1,500 kwa kilo 1 ya mchele.
Je ungehitaji kuuza au kununua mazao ya kilimo na mifugo? WhatsApp :0757 757 968.