Zao la pasheni jijini Mwanza kwa sasa (tarehe 15/11/2024) ni TZS 500 kwa tunda 1 sawa na TZS 5000 kwa kilo 1 kwani kilo moja hujaa matunda 10 -12 ya pasheni yenye ujazo wa gram 80-100 kwa kila tunda.
Msimu wa matunda haya kwa kanda ya ziwa ni kati ya mwezi Mei-Julai kila mwaka ambapo kilo moja ya pasheni au jina maarufu makakara huuzwa kati ya TZS 2000 - 3000.
Matunda ya pasheni yanayouzwa jijini Mwanza kwa kiasi kikubwa hutoka katika mkoa wa Kagera na Kigoma.
Je unahitaji kuuza au kununua mazao ya kilimo na mifugo?