MASOKO YA NAFAKA YAPETA ! MAHARAGE YAELEKEA KUSHUKA
Share
Leo 8/11/2024 kuelekea mwisho wa mwaka mazao ya nafaka bei hupanda na kufikia kiwango cha juu kabisa mwezi Desemba kila mwaka.Hivyo kama uliweka mazao yako stoo huu ndio muda wa kuyatoa;ndio kipindi cha kuvuna ulichopanda;bei sasa ni nzuri kwa mazao ya nafaka na huenda ikazidi kuwa nzuri kwa mkulima na mbaya kwa yule mlaji wa mwisho.Ni mchezo wa kuoteana ndio maisha yalivyo.
TAARIFA YA MASOKO YA NAFAKA BUKOBA MJINI LEO TAREHE 8/11/2024
Kiroba cha kilo 25 cha unga wa sembe ni TZS 28,000 kwa jumla ;wastani wa TZS 1200 kwa kilo ya sembe katika maduka ya rejareja.Huku mchele wa kawaida ukiuzwa TZS 74,000 kwa kila kiroba cha kilo 50 ambayo ni wastani wa TZS 1500 kwa kilo ya mchele katika maduka ya rejareja.Hivyo bei ya mchele na unga wa sembe inaenda sambamba.Unga wa dona ni TZS 22,000 kwa kiroba cha kilo 25.
Mavuno ya maharage yameanza kwa ukanda wa magharibi katika mikoa ya Kigoma na Kagera na hivyo bei ya maharage imeanza kuteremka;bei ya jumla ya maharage ya njano mjini hapa kwa sasa ni TZS 2600 kwa kilo 1;kabla ya mavuno kuanza bei ilifikia TZS 3000 kwa kilo.
Ungehitaji kujua bei ya zao gani ? Bofya alama ya WhatsApp na upate majibu mara moja!
AJE-FARMS MASHAMBA YANAYOTEMBEA.