MWANAMKE MWENYE NDOTO YA KUWA BILIONEA KUPITIA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI
Share
Asbuhi moja ya jumapili tulivu ya mwezi wa 10 ya mwaka 2024 napokea simu na kuitikiwa na sauti ya mwanamke aliyejitambulisha kwa lafudhi ya Kisukuma akiwa amechangamka na kwa kujiamini na anasema:- " Mimi naitwa Rahel Petro Emmanuel ninaishi katika Kijiji Cha Ngh'aya kilichopo kata ya Ngh'aya wilaya ya Magu mkoani mwanza ;nimeona kuhusu mradi wa AJE-FARMS mtandaoni na ningependa kujua kama naweza kupata soko la kuku wa kienyeji kwenu? Utaratibu upoje?"
"Naam",naitikia na kumkariibisha AJE-FARMS MASHAMBA YANAYOTEMBEA na kumueleza kuhusu huduma na bidhaa zetu;namuelezea kuhusu mradi wa shamba darasa -mradi wenye lengo la kutoa elimu ya kilimo na ufugaji pamoja na kuwasaidia wakulima kuyafikia masoko ya ndani na nje.
Na mara baada ya maongezi yetu katika simu kwa dakika zipatazo 10 hivi nilimsihi tuchat kwa WhatsApp ili nipate kujua kwa kina mradi wake. Kisha ndani ya siku kadhaa tuliendelea kuwasiliana na akapatiwa oda za kuku kuwatuma kwa wateja katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Dar es Salaam na Morogoro.Kuku waliisha ndani ya siku chache tu na akalazimika kuanza kukusanya kuku wengine kutoka kwa wafugaji wenzake ;na hapo ndipo akawa na nia ya kujua zaidi kuhusu mradi wa shamba darasa.Basi na mimi nilimuomba aandike historia ya mradi wake na tulikubaliana kuwa historia yake ingechapishwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ili kuhamasisha na kuelimisha vijana na wanawake wengine wengi ambao bado hawajaona fursa hii ya ufugaji wa kuku wa kienyeji kibiashara.
Naye kwa roho yake ya kujitoa na kusaidia wengine aliandika historia yake kwa njia ya ujumbe kupitia mtandao wa WhatsApp kama ifuatavyo:-
"Mimi ninaitwa Rahel ,Kitaaluma Mimi ni Mwalimu,nikiwa Mwalimu pia huwa ninajishugulisha na Kilimo Cha Mpunga na ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa takribani miaka mitano sasa.
Nilianza na kuku wachache tu jogoo na tetea wawili baada ya muda wa miezi miwili waliongezeka idadi ndipo nilipo pata wazo la kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku wa kienyeji na nifuge kama biashara yangu ya nyumbani ili iweze kunipatia kipato cha ziada katika familia yangu.
Kwanza ilinibidi nionane na mtaalamu wa mifugo hapa kijijini kwetu nikaomba ushauri wa namna nzuri ya kufuga kuku wa kienyeji alinipa mwongozo kwa kuzingatia mambo yafuatayo:-
1:Kuwapa kuku lishe Bora ili waweze kutaga mayai mengi hadi mayai ishirini kwa kuku mmoja
2:Kutambua yai lillilo Bora ili kupata vifaranga vilivyo Bora
3: Jinsi ya kulea vifaranga kwa kuwatoa kwa mama yao baada ya kutotolewa kwa kutumia jiko la mkaa
4: Kutunza vifaranga kwa kuwapa lishe Bora ili wasipatwe na magonjwa
5: Kuzingatia chanjo ya vifaranga na kuku wote kwa usahihi kuanzia siku ya kwanza (1_28) na kuendelea
6: Kuzingatia usafi wa Banda wanapo lala kuku
Katika hatua hii ya ufugaji wa kuku wa kienyeji kuna changamoto ambazo hujitokeza mfano
1:Upatikanaji wa chanjo kwa wakati Kuna wakati mwingine unahitaji kuchanja lakini chanjo husika inakosekana
katika mazingira yetu inasababisha vifaranga na kuku wengine kufa
2:Gharama za kununua lishe ya vifanga au chakula Cha vifaranga waliotolewa kwa mama yao baada ya kutotolewa
3: Upatikanaji wa soko la kudumu la kuuzia kuku wa kienyeji kwa wakati
Kutokana na changamoto hizi ndipo nilipoamua kuwatembelea majirani zangu na kuwashirikisha kuhusu njia gani tutumie ili tuweze kupata namna nzuri ya kupata chanjo kwa wakati
Tulikubaliana kuchangia gharama kwa Kila chanjo husika na mmoja wetu anaenda kununua inakopatikana pia tukashauriana kushirikishana katika Upatikanaji wa soko pale linapo patikana .
Siku moja katika kutafuta soko la kuuzia kuku wa kienyeji mtandaoni nikaiona chaneli ya AJE FARMS MASHAMBA YANAYOTEMBEA nikawauliza kuhusu soko la kuku wa kienyeji wakanipa mwongozo wa kuuza kuku wa kienyeji kwa njia ya mtandaoni.
Kiukweli haikuwa rahisi kuamini kuwa ni sehemu sahihi ilibidi nimshirikishe na mume wangu naye pia hakuamini kwa kuhisi ni utapeli wa mitandaoni.
Lakini AJE FARMS walinipigia simu na kunitoa wasiwasi wakaniambia kuwa hii ni kampuni sio mtu binafsi tunafanya biashara ya masoko mtandaoni ya kuuza na kununua bidhaa mbalimbali za kilimo na ufugaji.
Muda nikiwa sijaamini walinipa tenda ya kusafirisha vifaranga vya kuku wa kienyeji lakini kwa vile nilikuwa sijaamini tenda hiyo ilinipita.
Ilinibidi kuchukua hatua ya kuthubutu""niliwarudia na kuwaambia nipo tayari kufanya nao biashara.
Kwa kweli AJE FARMS walinipa moyo sana juu ya soko la kuku wa kienyeji. AJE FARMS walinisaidia kuuza kuku wangu kwa muda mfupi tuu wakaisha hadi ilinibidi kuwaunganisha na wafugaji wengine katika jamii yangu inayonizunguka kujiunga na AJE-FARMS ili kupata soko kwa uhakika.
Kupitia AJE-FARMS MASHAMBA YANAYOTEMBEA nimepitia mafanikio ambao hata sikutarajia kuyapata nimenunua mashine ya kutotoreshea mayai yenye uwezo wa kutotoreshea mayai 112 kwa wakati mmoja; hii itanisaidia kukuza kipato cha familia yangu na hata kwa wanajamii wenzangu kwani wataweza kutotoresha mayai yao kisasa na kuepuka upotevu wa mayai uliokuwa unajitokeza kwa kuatamia kuku kwa njia za asili kwani wakati mwingine mayai huharibika na huchelewesha uzalishaji na kukuza mradi wa ufugaji wa hawa kuku wa kienyeji.
Matarajio yangu katika hatua hii ya ufugaji natamani sana kuwa bilionea wa ufugaji mkubwa wa kuku wa kienyeji na hata ikiwezekana niwe mfugaji wa kimataifa wa kuku wa kienyeji ili niweze kutoa ajira kwa vijana ambao wapo mtaani na hawana ajira ili waweze kunipatia kipato kupitia mradi wa kuku wa kienyeji.
Wito wangu kwa wanajamii yote na wafugaji wadogo wadogo wa kuku wa kienyeji tuwe na uthubutu wengi wetu tunaogopa kuwa ufugaji una gharama lakini niwatoe wasiwasi Sasa hivi soko liko wazi kupitia AJE FARMS MASHAMBA YANAYOTEMBEA tuzingatie ufugaji wa kisasa ili mifugo yetu iweze kuwa na kiwango kizuri kinacho hitajika katika masoko.
Wito kwa serikali na kwa wadau binafsi itushike mkono hasa sisi wanawake tupatiwe mikopo yenye masharti nafuu ili tuinue mitaji yetu na hivyo tuweze kuwekeza kwenye miradi mikubwa ya ufugaji wa kuku wa kienyeji kama baadhi ya wafugaji wanavyofuga kuku wa kisasa ambao soko lake linaanza kushuka kutokana na hofu ya ongezeko la vyakula vya vinavyozalishwa kwa madawa na kemikali nyingi zinazotishia afya ya mwanadamu na ikolojia ;kwa namna hii tutafuga kuku kienyeji, kuboresha afya na kulinda mazingira yetu huku tukijikwamue kiuchumi.
Pia itanisaidia mwanamke kutokuwa tegemezi katika familia kwani ni mradi rahisi ataweza kuhudumia familia kikamilifu na muda huohuo ataweza kuhudumia au kusimamia mradi wake wa ufugaji wa kuku wa kienyeji"
Je ungependa kuwasiliana moja kwa moja na mwanamke huyu shujaa ambaye hajaridhika na kipato cha mshahara wake badala yake ameamua kujishughulisha katika ufugaji wa kuku wa kienyeji akiwa na ndoto ya ya kuwa bilionea na hivyo kujikomboa kiuchumi,kulinda mazingira na kutengeneza ajira kwa vijana na wanawake wenzake? Ungependa kuutembelea mradi wake uliopo Magu ili kuweza kujifunza zaidi kutoka kwake? Tafadhali tuandikie maoni yako hapa .Au wasiliana nasi kwa WhatsApp:+255 757 757 968 :Email: info@aje-farms.com
Na Mwandishi Wetu -Mwanza.
1 comment
Mara nyingi tunakwama kufikia malengo kwa kukosa uthubutu, elimu juu ya kile unachoamua kufanya, masoko, walanguzi na matapeli na hivyo kufanya watu wengi kukata tamaa na kuishia njiani lakini nimpongeze sana mwalimu mwenzangu Rahel kwa hicho alichoamua kukifanya, asiache, apambane na kukaza uso kwenye lengo lake. Tuwe maskini kwa kujitakia tu lakini hakika fursa ni nyingi mnoooo, wa kuzifanya ndio hawapo na waliopo hawajui wafanyeje kukidhi kiwango Cha fursa husika.
Angalizo: Hakuna mafanikio kurupushi, mafanikio ni mchakato na hatua, kubali kuumia, kubali kuanguka na kuinuka tena, kubali kuchekwa, kubali kuonekana huna akili lakini ipo siku watakiri kwa vinywa vyao kuwa, “MWENZETU ULIONA MBALI.”
Kongole mwalimu Rahel.