Nyanya Yaendelea Kudoda Maeneo Mengi Nchini !
Share
Hadi kufikia leo tarehe 8/11//2024 soko la nyanya bado haliridhishi kabisa maeneo mengi nchini tofauti na matarajio ya walio wengi hasa kwa Mkoa wa Geita ambapo Wilayani Chato nyanya bado zinauzwa kwa mfumo wa kupima kwa ndoo badala ya kilo; jambo ambalo linamnyonya mkulima.Kwa takribani miezi 7 mfululizo bei ya nyanya wilayani hapa ni TZS 5000-10000 kwa ndoo yenye kilo 15-20;ambapo kwa kadirio kila kilo 1 imekuwa ikuzwa kwa TZS 250 kwa wastani.Bei ya chini wilayani humo pengine inachangiwa na uwepo wa wakulima wengi wa nyanya na huku pakiwa na viwanda vichache vya kusindika nyanya.Hata hivyo ukanda huu umekuwa ukipata baraka ya wanunuzi wa nyanya kutoka nchi ya Rwanda ambao bei yao kidogo imekuwa nzuri ikilinganishwa na soko la ndani ambapo Wanyarwanda hawa wamekuwa wakilangua nyanya moja kwa moja mashambani kutoka kwa wakulima kwa wastani wa TZS 35,000 kwa tenga lenye kilo 80. Ni dhahiri mkulima bado anaNYANYAsika !
Kwa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya bei ya nyanya ni TZS 15,000-17,000 kwa ndoo yenye kilo 15 -20 na hivyo bei angalau inatia matumaini kwa wakulima wilayani Chunya-Mkoani Mbeya.
Usikose kufuatilia taarifa na masoko ya mazao ya kilimo na mifugo kutoka maeneo mbalimbali kila siku na huku tukikusogezea fursa kabambe mlangoni kwako.
AJE-FARMS MASHAMBA YANAYOTEMBEA !