SOKO LA ZAO LA PARETO LAPETA KIMATAIFA

SOKO LA ZAO LA PARETO LAPETA KIMATAIFA

Katika kikao kilichofanyika Dodoma tarehe 07/11/2024 Mkurugenzi wa Zao la Pareto Nchini Bw.Lucas Ayo alisema bei ya zao la pareto limepanda toka shilingi 3,500 hadi shilingi 3,700 itakayoanza kutumika kuanzia tarehe 8 Novemba 2024.

Aidha Bw.Ayo amebainisha kuwa bei ya zao la pareto itakuwa na wigo wa kupanda hadi kufikia shilingi 5000 kwa kilo moja kutokana na ubora wa maua wa zao hilo,huku akiwasisitiza wakulima kuzingatia njia bora za kilimo.

Uzalishaji wa zao la pareto unatarajiwa kufikia takribani tani 10,000 hadi kufikia mwaka 2030.

Pareto iliingizwa na kuanza kulimwa kwa mara ya kwanza Tanzania mwaka 1931.

Zao hili la kibiashara hustawi vizuri katika Nyanda za juu za Tanzania.

Zao hili pia ni maarufu duniani kwa kuwa na maua yenye sumu aina ya kiua wadudu asili (Pyrethrins).

Sumu ya Pareto ina sifa kuu zifuatazo: Kuua wadudu kwa haraka baada ya kupata harufu yake; Inaua wadudu kwa jinsi ya pekee ikilinganishwa na sumu zinazotengenezwa viwandani;

Back to blog

Leave a comment