BANANA PLANTLETS -TISSUE CULTURE
BANANA PLANTLETS -TISSUE CULTURE
Hii ni miche iliyozalishwa kwa njia ya chupa katika maabara (tissue tissue) baada ya kuvuna meristem kutoka kwenye mashina ya migomba iliyovunwa kwenye mashamba mama ya migomba ambayo hutunzwa kwa umakini wa hali ya juu ili kuikinga na magonjwa ya migomba na ndizi. Teknolojia ya uzalishaji miche kwa njia hii ndio teknolojia ya juu kabisa na yenye gharama kubwa ikilinganishwa na uzalishaji wa vikonya na kwa njia ya macropropagtion. Miche iliyozalishwa kwa njia hii hukomaa kwa pamoja shambani au kwa tofauti ndogo sana na hivyo kumpa nafasi mkulima kuvuna ndizi nyingi kwa wakati mmoja.
Ikumbukwe uwekezaji wa kwanza katika kilimo cha migomba huanza na kuchagua miche bora.Wakulima wengi wamekuwa wakifanya makosa yanayofanana kwa kupata miche ya migomba bure au kwa bei ndogo wakihisi wameepuka gharama ya kununua miche bora kutoka katika vitalu vinavyoaaminika kumbe ndio wanaingia kwenye gharama kubwa sana baada ya kugundua kuwa migomba hiyo ilikuwa na magonjwa miezi kadhaa mara baada ya kuipanda shambani.Hapa inaonesha kilimo hakina mkato kabisa. Wakulima hawa wenye kupenda njia ya mkato hujikuta wakilazimika waking'oa mashina yote ya migomba shambani na kutakiwa kupanda upya au kubadilisha kabisa mradi na hata wakati mwingine kuyakimbia mashamba yao na kukichukia kilimo.
Ukitaka kufaulu katika kilimo biashara cha migomba sharti ununue miche bora kutoka katika vitalu vinavyoaaminika.
Unaalikwa kununua miche bora ya miche ya migomba aina zote iliyo katika mfumo wa vikonya vilivyovunwa katika mashamba yetu mama ya migomba (mother gardens) ili kufurahia kilimo cha migomba.
Na ukinunua miche kutoka kwetu utapatiwa kitabu cha kilimo cha migomba bure na kuunganishwa kwenye group ya WhatsApp ya kilimo cha migomba - yote bure na hivyo kujiunga katika familia pana ya wakulima na wafanyabiashara wa mazao ya ndizi.Vilevile utapata msaada wa kuyafikia masoko ya ndizi ukiwa shambani kwako kwa kusajiliwa kwenye mradi wetu wa shamba darasa.
Unasubiri lini?!
Agiza miche yako na uanze safari yako ya ukombozi kiuchumi kupitia kilimo biashara cha migomba. WhatsApp :+255 757 757 968 au tuandikie kwa Email: info@aje-farms.com kwa maelezo na msaada zaidi.
See you there !